NIJUZE NIJUZE Author
Title: PWANI: KIWANDA CHA NONDO KUIINGIZIA SERIKALI BILIONI 200 ZA KODI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Serikali inatarajia kukusanya sh.bilioni 200 kwa mwaka, ikiwa ni mapato ya kodi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha kimataifa cha...
Serikali inatarajia kukusanya sh.bilioni 200 kwa mwaka, ikiwa ni mapato ya kodi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha kimataifa cha Kiluwa Steel Group kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha tani 3,000 za nondo kwa siku.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na mwekezaji mzawa kwa kushirikiana na Wachina, inatarajiwa kukamilika Oktoba, mwaka huu ambapo fedha hizo zitapatikana baada ya kukamilika awamu tatu za ujenzi wake.

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyetembelea kiwanda hicho Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Mohammed Kiluwa alisema ujenzi huo utasaidia kuimarisha uchumi.

Kiluwa alisema, awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu, ambapo awamu ya tatu itakamilika Februari mwakani. Kikikamilika, kinatarajiwa kuajiri vijana zaidi ya 500 wa Kitanzania.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kikubwa cha kwanza kinachojengwa na mwekezaji mzawa.

Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda hicho katika eneo la Disunyara, Mlandizi mkoani Pwani, utawezesha kuboresha hali ya uchumi kwa wakazi wa eneo hilo na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu alitolea mfano kwa wakazi wa Mtwara, ambao wamenufaika kutokana na ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote ambapo awali walikuwa wakinunua saruji kwa sh.17,000, lakini hivi sasa wanainunua kwa sh. 7,000.

Chanzo: ITV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top