NIJUZE NIJUZE Author
Title: CCM YATOA KAULI HIZI HII NI BAADA YA CHADEMA KUTAJA SIKU YA MAANDAMANO
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
July 28 2016 Chama cha mapinduzi (CCM) kikiongozwa na msemaji wake Christopher Ole Sendeka kimekutana na waandishi wa habari Dar es sala...
July 28 2016 Chama cha mapinduzi (CCM) kikiongozwa na msemaji wake Christopher Ole Sendeka kimekutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kuzungumzia hatua iliyotangazwa na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kufanya maandamano ya nchi nzima.
Ole Sendeka
Ole Sendeka amesema 
"Jana tarehe 27/7/2016 chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), walitoa kauli iliyojaa uongo mwingi za kibabaishaji na kuthibitisha ukweli kuwa kwa hakika kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli na kufanya wapinzani kukosa ajenda"

"Katika uongo na uzushi walioutangaza, CHADEMA wanasema wameamua kufanya mikutano na maandamano nchi nzima, kimsingi hoja walizozitumia zimejaa upotoshaji na uongo uliokithiri. Ifahamike kuwa serikali haijazuia mikutano kwenye majimbo yao" - Ole Sendeka

"Wabunge wako huru kufanya shughuli zao na tumeona baadhi ya wabunge wakifanya shughuli zao majimboni bila shida wakiwemo hao wa upinzani" – Ole Sendeka

"Ni vizuri tukakumbuka matukio kwenye operesheni kama hizi yaliyopoteza maisha ya vijana wetu na matokeo ya kila operation" – Ole Sendeka

MSIKILIZE HAPA AKIFUNGUKA ZAIDI:

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top