
Nje ya mahakama hiyo Lissu alizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa kauli ambayo imewafanya polisi wamuite kwa ajili ya mahojiano, Lissu alisema….
"Nchi yetu inaingizwa kwenye giza nene na dikteta uchwara hatuwezi kuongozwa na mtu wa namna hiyo, hata kama kachaguliwa na kuwa Rais"
Mbunge huyo wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amehojiwa na polisi kwa saa tatu kutokana na kauli hiyo aliyoitoa jana nje ya mahakama ya Kisutu wakati akiongea na waandishi wa habari. hivyo Lissu atalala rumande leo kwa amri ya ZCO baada ya kukosa dhamana na atafikishwa mahakamani kesho.
Tags
HABARI ZA KITAIFA