SHILOLE AVULIWA NGUO KWEUPEE, MWENYEWE AZUNGUMZA MAZITO, KISA JIKE SHUPA

Msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameonesha masikitiko yake kufuatia madai ya kudhalilishwa na baadhi ya wasanii wenzake kwa kuipa promo video ya wimbo mpya wa zilipendwa wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ wa Jike Shupa.
Zuwena Mohammed
Kwa mujibu wa Shilole, video ya wimbo huo inaonesha matukio ya kumdhalilisha ambayo inaonekana yeye alikuwa akimfanyia Nuh enzi za uhusiano wao kama vile kumpiga na kumzodoa, mambo ambayo hakuwahi kuyafanya.
“Nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya wasanii wenzangu kuiposti video hiyo kwenye mitandao mbalimbali, huko ni kunidhalilisha kwa sababu jamii ikiangalia inaweza kunitafsiri tofauti,” alisema Shilole.

Katika video hiyo, msichana anayefanana na Shilole aitwaye Zuwena aliyetumika kama video queen anaonekana akimfanyia vitimbi Nuh huku akitafsiriwa kuwa, ndivyo Shilole alivyokuwa akimfanyia jamaa huyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post