NIJUZE NIJUZE Author
Title: SHILOLE ATOKWA POVU KISA VIDEO YA "JIKE SHUPA" TAZAMA HAPA ALICHOKIFANYA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Ikiwa ni siku chache toka Ex wa Shilole , Nuh Mziwanda aachie video ya wimbo ‘Jike Shupa’ ambayo inaelezea jinsi alivyoishi na mpenzi ...
Shilole
Ikiwa ni siku chache toka Ex wa Shilole, Nuh Mziwanda aachie video ya wimbo ‘Jike Shupa’ ambayo inaelezea jinsi alivyoishi na mpenzi wake huyo, Shilole ameonyesha kukasirishwa na kazi hiyo.

Nuh amethibitisha kwamba Shilole ndiye aliyemuimbia kwenye wimbo huo, kwa kumtumia video queen anayefanana na Shilole kama pacha katika video ya wimbo huo.

Jike Shupa
Video queen wa video ya wimbo ‘Jike Shupa’ anayedaiwa kufanana na Shilole akiwa na Nuh

Sholole baada ya kuona video hiyo, aliandika ujumbe Instagram ambao baada a muda mchache aliutoa:

Wale unaongozana nao wanaweza kuwa mizigo au Baraka. Shukrani za dhati kwani kwenye mashabiki zangu ambao ni baraka na pole sana wasanii wote mnaodhani bado tupo dhama za kutumia mgongo wa mtu mwingine kuweza kutoboa. Kipaji siyo maneno ila ni vitendo. Umemiss mkong’oto?. Sipendagi mwanaume mjinga ndiyo maana umekula mkong’oto wa kutosha… Mshamba usiyejua hata kubadilisha boxer, niweke mbali na maisha yako. Nikifungua mdomo wangu utadhalilika."
Shilole na Nuh Mziwanda waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo Nuh amekuwa akizungumzia mengi yaliyomkuta wakati akiwa kwenye mahusiano na mwanadada huyo, huku Shilole akikataa kuzungumzia kilichotokea.

Hii ndiyo video ya wimbo Jike Shupa

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top