NIJUZE NIJUZE Author
Title: SHILOLE - "HAKUNA MZURI KAMA MIMI KWA WASANII WA BONGO FLEVA, NEDY MUSIC HUNIFANYA NISMILE MUDA WOTE"
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Msanii Shilole ambaye haishi vituko kwa mashabiki wake amejigamba kuwa kwa Bongo hakuna msanii mzuri kama yeye, kwani ana uzuri wa asili si...
Msanii Shilole ambaye haishi vituko kwa mashabiki wake amejigamba kuwa kwa Bongo hakuna msanii mzuri kama yeye, kwani ana uzuri wa asili sio ule wa kutumia vipodozi.
Shilole
Shilole ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na EATV.

"Mimi ni mwanamke mzuri without make up (bila vipodozi), unaweza ukaniamsha usingizini na nikaenda popote bila makeup, katika Bongofleva mimi ni mwanamke mzuri sana hamna anayebisha,” alisema Shilole.

Pamoja na hayo Shilole amezungumzia suala la kuwa na ukaribu na msanii Nedy Music, na kusema kuwa msanii huyo ni rafiki yake tu na si vinginevyo. “Nedy ni mshkaji wangu tu, ananifanya nismile,” alisema Shilole.

Pia Shilole amesema Jumatatu ya wiki ijayo anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaoitwa 'Say ma Name'.

About Author

Advertisement

 
Top