
Mh Suluhu ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni ya longa nasi ambayo inatoa fursa kwa wananchi kutumia mitandamo mbalimbali ya simu kutoa taarifa mbalimbali zinazohusina na rushwa.
Naye waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejinment ya utumishi wa umma na utawala bora Mh Angela Kairuki ameitaka Taasisi ya Kuzuia na na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kuongeza kasi katika utendaji kazi wake ila ifanye kazi bila ya kumuonea mtu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola amesema wananchi wanaruhusiwa kupiga simu bure Kupitia namba 113 katika mitandao yote ya simu za mikononi na tarifa zao zitapokelewa na kufanyiwa kazi kwa umakni mkubwa kabisa.
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika uzinduzi huo wamezungumza namna watakovyonufaika na mfumo huo huku Jakson Mmbando mwakilishi wa makampuni ya simu yeye akitokea Airtel akisema wamejipanga vyema kuhakisha kuwa wananchi wanatumia huduma hiyo bure ili kuweza kutoa taarifa zao kwa urahisi.
Tags
HABARI ZA KITAIFA