HATIMAE BONDIA MANNY PACQUIAO APATA USHINDI NAFASI YA USENETA NCHINI UFILIPINO

Bondia Manny Pacquiao May 19 amefanikiwa kushinda nafasi ya Seneta katika bunge la nyumbani kwao Ufilipino. Amefanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kura milioni 16.
Manny Pacquiao
Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 anakuwa miongoni mwa watu 12 walioshinda nafasi ya Seneta katika bunge la Ufilipino. 

Ushindi huu kwa bondia huyo unatoa taswira huenda siku moja akapata nafasi ya kugombea nafasi za juu za uongozi wa nchi hiyo hususani Urais.
Previous Post Next Post