“Kiukweli nimemiss kuimba gospel....naimba moyoni mwangu ila nimemiss kusimama ile kwa watu, actualy inahitaji watu kuelewa kwamba ninachofanya ni biashara na kama kazi nyingine”, alisema Rubby.
Ruby aliendelea kusema mpaka sasa hajawahi kusimama na kuimba kwenye kanisa lolote na hajajaribu, kwani kwenye makanisa hayo anahisi kuna unafiki.
“Unajua kuna makanisa mengine ukiingia unafeel presence of God, lakini mengine una-feel unafiki, kwa kweli kibongo bongo yale makanisa ya kusema wamuite msanii wa bongo fleva aimbe bado hakuna”, alisema Ruby.