CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha Mjini kimepata ushindi wa viti vitano dhidi ya vitatu vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwenye uchaguzi wa wenyeviti wa serikali ya mtaa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu wa CCM wilaya ya Arusha Mjini, Feruzi Bano alisema ushindi huo unatokana na kasi ya Rais John Magufuli ya utumbuaji majipu, ambayo imewakuna wananchi wengi na kuanza kupenda chama hicho tawala.
Bano alitaja mitaa ambayo CCM imeshinda ni mtaa wa Olamuriaki kata ya Sombetini na mtaa wa Shangarau kaya ya Moivaro, ambapo katika mitaa yote hiyo, CCM imepita bila kupingwa baada ya Chadema kushindwa kusimamisha wagombea.
Mitaa mingine ambayo CCM imeshinda ni mtaa wa Makao Mapya kata ya Sinoni, mtaa wa Bondeni kata ya Kati na mtaa wa Kilimaji kata ya Moshono. Kwa upande wa wajumbe wa serikali za mitaa, alisema CCM ilipata wajumbe watatu huku Chadema ikipata mmoja.
Alisema, mvua kubwa iliyonyesha juzi ilifanya baadhi ya wapiga kura wao hususani wenye umri mkubwa, wakashindwa kwenda kupiga kura.
Sababu nyingine ziliyoathiri uchaguzi huo ni karatasi za kupigia kura kutokuwa na muhuri wa Halmashauri ya Jiji na kutokuwepo kwa vitambulisho vya kuonesha kama kweli waliopiga kura katika mitaa hiyo walikuwa wakazi husika.
Katika mtaa wa Sanare Kata ya Daraja Mbili, wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali ya mtaa kwa vyama hivyo viwili, walifungana hivyo uchaguzi utarudiwa. Msimamizi wa Uchaguzi, ambaye ni mkurugenzi wa Jiji, Juma Iddy anatarajiwa kutangaza tarehe nyingine ya uchaguzi.
Uchaguzi huo ulifanyika juzi kutokana na wenyeiti wa mitaa tisa, kuhamia vyama mbalimbali vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.