YANGA YASONGA MBELE CAF CHAMPIONS LEAGUE, BAADA YA KUTOKA SARE TAIFA

MABINGWA watetezi Tanzania Bara Yanga SC Leo wakiwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakicheza Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Armee Patriotique Rwandaise FC walitoka Sare 1-1 na kusonga Raundi ijayo kwa vile walishinda Mechi ya Kwanza Bao 2-1.

Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Kigali, Rwanda, Yanga iliitandika APR Bao 2-1 kwa Bao za Juma Abdul na Thaban Kamusoko.

Leo Yanga walianza vibaya kwa kupigwa Bao Dakika ya 4 tu lakini Donald Ngoma akasawazisha Dakika ya 28 na kuwaingiza Raundi ya mwisho ya mtoano ambayo watapambana na Mshindi kati ya Al Ahly ya Egypt na Recreativo de Libolo ya Angola ambazo nazo Leo zinacheza Mechi ya Pili huko Borg El Arab Stadium Mjini Alexandria Nchini Misri baada kutoka 0-0 huko Angola.

MATOKEO YA MECHI ZA CAF CHAMPIONS LEAGUE
**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili

Cnaps Sports (Madagascar) 2-1 Wydad Athletic Club (Morocco) [3-6]
Vitalo FC (Burundi) 2-1 Enyimba International FC (Nigeria) [3-6]
Young Africans (Tanzania) 1-1 Armee Patriotique Rwandaise FC (Rwanda) [3-1]
Previous Post Next Post