KUTOKA ZANZIBAR:: MWANDISHI WA HABARI WA DW ATEKWA, SAUTI YAKE YASIKIKA AKIWA AMEFICHWA

Salma Said
Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle (DW-Swahili), Salma Said jana alikamatwa na watu wasiojulikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Unguja, alipokuwa akisafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia afya yake.

Akizungumzia tukio hilo jana, mume wa Salma, Ali Salim Khamis ambaye pia ni Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), alisema alipata ujumbe wa maandishi kutoka kwa mkewe kwamba amekamatwa.

Khamis alisema alipokwenda uwanja wa ndege aliambiwa na mkuu wa polisi wa uwanjani hapo kwamba hana taarifa za tukio hilo jibu ambalo alilipata pia kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi.

Alisema aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambako pia aliambiwa hawana taarifa za kukamatwa kwa Salma. “Hadi sasa sijui mke wangu yuko wapi bado naendelea kumtafuta.”

Unaweza kusikiliza Mahojiano ya DW na Salma Said akiwa sehemu ambayo haijulikani
Previous Post Next Post