BAADA YA KUAPISHWA MEYA WA JIJI ASEMA AKUBALIANI NA BOMOA BOMOA (+AUDIO)

Meya wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita leo amekula kiapo cha utiifu kulitumikia jiji la Dar es salaam mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya sokoine Drive Aziza Kali katika Ukumbi wa Karimjee jijini humo.
Isaya Mwita
Mara baadaVya kuapishwa Isaya Mwita amesema kuwa kitu cha kwanza hakubaliani na bomoa bomoa suala ambalo limegharimu maisha ya Watanzania wengi, isipokuwa atakubaliana nalo pindi atakapo pata taarifa za atakaye bomolewa ataelekea wapi.
“Hii ni nchi yetu wote kwakweli inaumiza sana pale unapoona mtu kajenga kibanda chake kwa muda mrefu na kinakuja kubomolewa baadaye je wakati huo serikali walikuwa wapi kwakweli inaumiza na katika Jiji langu sitakubaliana nalo”. Alisema Meya

Aidha ameongeza kuwa mji umekithiri uchafu kutokana na hali hiyo dampo moja halitoshi hivyo basi tutaongeza madampo kila wilaya katika wilaya zote ndani ya jiji na hayo yatatekelezeka endapo kila mmoja atalipa kodi kwa wakati kwani bila kulipa kodi hakuna maendeleo popote pale.

Unaweza kuisikiliza Sauti ya Meya Isaya Mwita hapo chini wakati akila kiapo cha uaminifu na utiifu.
Previous Post Next Post