NIJUZE NIJUZE Author
Title: WAKAZI WA KATA YA NAMAYUNI-KILWA MASOKO WAPONGEZA MTANDAO WA SIMU ZA MKONONI WA HALOTEL.
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Afisa habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kil...


halo kilwa

halo kilwa
Afisa habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.
halo kilwa
Mtaalamu wa masuala ya mtandao wa kampuni ya Halotel, Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Sebastian Inocent akifafanua changamoto mbalimbali zinazo wapata wakazi wa kijiji cha Namayuni.

Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Halotel ndio mtandao pekee unaotoa huduma za mawasiliano kwa njia ya Simu za mkononi katika kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi.


Mtandao huu ndio unawasaidia wakazi wa kata ya Namayuni kuweza kuwasiliana na ndugu na jamaa wa maeneo hayo na sehemu nyingine kwa njia ya simu ya mkononi kwa kuwa wamejengewa mnara unao wawezesha kuwasiliana kwa njia simu za mkononi.

Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura amepongeza mtandao wa simu za mkononi wa Halotel na kusema kuwa umeisaidia sana jamii ya wakazi wa kata ya Namayuni mkoani humo kutokana na hapo awali kutokuwepo na mtandao wowote wa simu.
" Tunawashukuru sana Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kukumbuka kama kunaviumbe huku na kutuwekea mnara katika kata yetu kwakua kabla ya mtandao huu tulisafiri na kupanda juu ya vilima ili kutafuta mtandao(network) ili tuweze kuwasiliana na watu wengine kwa njia ya simu."

Nao wakazi wa Kijiji cha Namayuni wamesema kuwa Mtandao huu wa Halotel "umetusaidi sana katika huduma mbalimbali hasa kutufichia siri katika mawasiliano kwani tulikuwa tunaenda umbali mrefu kwenda kutafuta mtandao, kwa sasa tunakaa ndani tuu na tunawasiliana na ndugu na jamaa bila mtu yoyote kujua kama tumewasilana na nani".

Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.

About Author

Advertisement

 
Top