JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - TAMISEMI
TAARIFA KWA UMMA
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kwa Mamlaka aliyopewa chini ya
Kifungu cha 2(2) cha Amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka
(DART), (The Executive Agencies) (The Dar Rapid Transit Agency)
(Establishment) Order ) Tangazo la Serikali namba 120 la 2007, amemteua
Mhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi
Yaendayo Haraka Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe 04/01/2016.
Uteuzi
huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa
Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe 23/12/2015. Kabla ya uteuzi
huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya
Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) akishughulikia Ufuatiliaji na
Tathmini. Mhandisi Lwakatare anatakiwa kuripoti na kuanza kazi mara
moja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Januari 05, 2016.
Tags
HABARI ZA KITAIFA
