Zitto kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook amefichua kuwa atahakikisha anapambana ili suala hilo linajibiwa kikamilifu na kwamba pesa zote ambazo Serikali inawadai wamiliki wa mitambo ya IPTL zinarudishwa kwa wananchi
“Juzi nimewasilisha maswali 5 Bungeni ili yajibiwe na Serikali. Swali la kwanza linahusu umiliki wa IPTL na tshs 8 bilioni tunazowalipa matapeli hao kila mwezi, kwanini mtambo haujamilikishwa TANESCO na anayejiita mmiliki wa IPTL kukamatwa na kushtakiwa. Vile vile ni kwanini Benki ya Stanbic haijachukuliwa hatua kwa kuamuriwa kurudisha Fedha za akaunti ya #TegetaEscrow. Mambo 2 ( umiliki wa IPTL na kurudisha kwa fedha tshs 320 bilioni) ndio mambo ya msingi kabisa katika suala zima la #TegetaEscrow. Haya ndio nitakufa nayo.”
POST YA ZITO KATIKA AKAUNTI YAKE YA FACEBOOK
Juzi nimewasilisha maswali 5 Bungeni ili yajibiwe na Serikali. Swali la kwanza linahusu umiliki wa IPTL na tshs 8...
Posted by Zitto Kabwe on Wednesday, December 16, 2015