Sumaye akionyesha Kadi ya Chadema mara baada ya kukabidhiwa
WAZIRI Mkuu mstaafu wa awamu ya Tatu, Frederick Sumaye ametangaza rasmi kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kukabidhiwa na kadi ya uanachama wa chama hicho.
WAZIRI Mkuu mstaafu wa awamu ya Tatu, Frederick Sumaye ametangaza rasmi kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kukabidhiwa na kadi ya uanachama wa chama hicho.
Sumaye, ambaye alijiunga na vyama vya Upinzani vinavyounda Ukawa miezi minne iliyopita wakati wa Kampeni za uchaguzi mkuu uliomalizika Octoba 25 mwaka huu, ambapo wakati huo Sumaye alikihama chama cha Mapinduzi CCM huku akishindwa kuweka wazi chama kipi alikiunga nacho.
Sumaye ametangaza hatua hiyo leo mkoani Arusha wakati wa kuhitimisha Kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Arusha mjini, ambapo amesema amejiridhisha pasipo shaka kuwa Chadema ndiyo chama pekee chenye kuweza kumletea maendeleo Mtanzania jambo lilofanya akihamie chama hicho huku akimpongeza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kuwa ndiye anayeweza kukijenga chama bila kutetereka.