NIJUZE NIJUZE Author
Title: TAZAMA PICHA ZA UZINDUZI WA MELI MPYA YA MV MAPINDUZI II MJINI ZANZIBAR LEO
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Picha ya Meli MV-Mapinduzi II ilipokuwa katika hatua za matengenezo Nchini Korea Kusini.   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza...
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Picha ya Meli MV-Mapinduzi II ilipokuwa katika hatua za matengenezo Nchini Korea Kusini.
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto)akikata utepe kama ishara rasmi ya uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II katika bandari ya Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar akiwepo na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kulia) Nahodha wa Meli hiyo Abubakar Mzee (kulia) na Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mabaharia waMeli ya MV-Mapinduzi II baada ya uzinduzi rasmi uliofanyika leo katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar,pamoja na kuitembelea kukagua sehemu mbali mbali za meli hiyo akiwa na Viongozi mbali mbali
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na wafanyakazi wa Kike katika Meli ya MV-Mapinduzi II wakati alipokuwa akifanya ukaguzi na kutembelea sehemu mbali mbali za Meli hiyo akiwa na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao baada ya uzinduzi rasmi uliofanyika leo katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakipata maelezo kutoka kwa Nahodha wa Meli ya MV-Mapinduzi II Abubakar Mzee (katikati) wakati walipofika katika chumba maalum cha mitambo ya kuendeshea meli inapokuwa safarini,maelezo hayo yalitolewa katika shamra shamra za sherehe za uzinduzi uliofanyika leo katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Mitambo mbali mbali ya Umeme katika Meli ya Mv-Mapinduzi II ikiwa katika hali ya Kuvutia kabisa kutokana na upya wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alitembelea sehemu hii wakati wa uzinduzi wa Meli hiyo iliofanyika leo
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Nahodha wa Meli ya MV-Mapinduzi II Abubakar Mzee (kushoto) wakati alipotembelea Chumba cha Abiria Classi ya Kwanza akiwa katika ukaguzi wa sehemu mbali mbali baada ya uzinduzi rasmi uliofanyika leo katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Katika Meli ya MV-Mapinduzi II kunapatika vifaa mbali mbali vya ukokozi ikiwemo moja ya aina hii ya Boti kama inavyoonekanwa ikiwa na mashine yake pamoja vifaa vyengine vya kutoa huduma.
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake kwa wananchi katika sherehe za uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II leo katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar,(kulia) Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee na Naibu Waziri wa Muindombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi Gavu (kushoto).
Picha zote na Ikulu, ZnZ
uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II
Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wananchi katika sherehe za uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II leo katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar 

About Author

Advertisement

 
Top