Wakazi wa Manispaa ya Lindi wamelalamikia Kitendo cha Baadhi ya Viongozi wa Serikali Kutumia Gari la Pekee la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya Kupelekewa Huduma ya Maji katika Majumba yao na Kusababisha Gari hilo kupata ajali likiwa katika Harakati hizo Tofauti na Matumizi ya Gari hilo.
Gari hilo la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji lenye namba za Usajili STK 3699 Majira ya Mchana limepinduka katika Maeneo ya Mtanda Lindi Mjini na kusaidia wakazi wa Maeneo hayo Kunufaika na Upataji wa Huduma ya Maji baada ya Kukosa Kwa Muda Mrefu.
Kufuatia Tukio hilo Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Lindi wameeleza Kusikitishwa kwao kwa Hatua hiyo ya Gari la Zimamoto Kuonekana mara kwa Mara Likitoa huduma kwa baadhi ya Viongozi wa Serikali huku mara Nyingine kuchelewa kufika katika Tukio kwa ukosefu wa maji au Ubovu Saidi Mnyengema Akielezea Tatizo kubwa la Maji
LindiYetu.Com Ilifika katika Ofisi za Zimamoto ili Kupata Ukweli wa Madai ya wananchi kuhusiana na Matumizi yasiyo halali ya Gari hilo na Kusababisha gari kupata ajali wakati likiwa katika harakati za kushusha maji nyumbani kwa katibu Tawala Mkoa wa Lindi.
Lakini Harakati Hizo hazikuzaa Matunda Baada ya Mkuu wa Kikosi Hicho Mkoa wa Lindi, Mkaguzi Abbas Mnyenyelwa kudai kutopata Maelezo kamili kwa mkuu wa Kituo na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa.
Kupata Ajali kwa Gari Hilo Kutaathiri kwa Kiasi kikubwa kati Mji wa Lindi Ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kikwetu ikitokea Dharura ya Kutua au kuruka kwa Viongozi wa Kitaifa wanaotumia Uwanja huo.

Kufuatia Tukio hilo Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Lindi wameeleza Kusikitishwa kwao kwa Hatua hiyo ya Gari la Zimamoto Kuonekana mara kwa Mara Likitoa huduma kwa baadhi ya Viongozi wa Serikali huku mara Nyingine kuchelewa kufika katika Tukio kwa ukosefu wa maji au Ubovu Saidi Mnyengema Akielezea Tatizo kubwa la Maji

Lakini Harakati Hizo hazikuzaa Matunda Baada ya Mkuu wa Kikosi Hicho Mkoa wa Lindi, Mkaguzi Abbas Mnyenyelwa kudai kutopata Maelezo kamili kwa mkuu wa Kituo na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa.

Tags
HABARI ZA KITAIFA