NIJUZE NIJUZE Author
Title: KIFO CHA MEMBER WA GHETO KIDS, CHA MGUSA MSANII HUYU MKUBWA WA NIGERIA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Msanii Patoran King kutoka nigeria ameelezea hisia zake baada ya kupata taarifa za kifo cha mtoto Alex wa Ghetto kids, ambaye alijipatia um...
Msanii Patoran King kutoka nigeria ameelezea hisia zake baada ya kupata taarifa za kifo cha mtoto Alex wa Ghetto kids, ambaye alijipatia umaarufu duniani kwa kucheza wimbo wa Sitya Loss wa msanii wa Uganda Eddy Kenzo.
Alex Ssempijja
Marehemu Alex Ssempijja wa Ghetto Kids

Patoran King ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa amehuzunishwa na msiba huo na kwamba Alex alikuwa mchezaji mwenye kushangaza kwa umahiri wa wake, na kumuombea heri Mungu ampumzishe salama.
Patoran King
"Am in tears Right now but God knows best,Life is too short to Hate,to grudge and badmind another man, Alex sitya Loss, is an amazing dancer from Uganda,he's with a group called Ghetto kids cc @eddykenzo he died in an accident few days back May God bless soul...Rest in Power Alex,God bless the Ghetto kids..be strong @eddykenzo", aliandika Patoran King kwenye ukurasa wake akimaanisha........"Niko kwenye machozi sasa hivi lakini Mungu anajua zaidi, maisha ni mafupi sana kuchukia, kuwa na nafsi mbaya, Alex Sitya loss alikuwa mchezaji wa kushangaza kutoka Uganda, yuko kwenye kundi linaloitwa Ghetto Kids, amefariki kwenye ajali siku chache zilizopita , Mungu abariki nafsi yake, Mungu awabariki Ghetto kids..kuwa na nguvu Eddy Kenzo".
Eddy Kenzo na  Alex
Eddy Kenzo akiwa marehemu Alex enzi za uhai wake.
Alex Ssempijja alifariki juzi na kuzikwa jana, baada ya kupata ajali walipokuwa wakiendesha baiskeli yeye na mtoto mwenzake Patricia, ambaye naye yuko hospitali akipatiwa matibabu.

About Author

Advertisement

 
Top