Kajala amesema mwaka 2015 ametayarisha filamu nyingi lakini ameshindwa kuzitoa kutokana na soko la filamu kusuasua.
“Siwezi sema kwangu kuna tatizo ni kujipanga tu licha ya changamoto za wezi wa kazi zetu ambao wanatukatisha tamaa,” alisema.
“Lakini nashukuru kuona serikali tayari imeanza kurudisha matumaini kwa kujaribu kuweka sheria ili tupate haki zetu kwa sababu wasanii wengi walikuwa wazito kufanya kazi kwa sababu wanaona hata nikifanya sipati yale mafanikio ambayo nahitaji,” aliongeza.
“Mimi nina movie nyingi nitaanza kuzitoa mwaka 2016 mwanzoni kwa sababu tayari tumeshaanza kuona dalili za kile tunachokihitaji.”

Kajala na Quick Raka
Muigizaji huyo amesema kuwa mwaka 2016 utakuwa ni mwaka mzuri kwa kuwa tayari ana kazi ndani ambazo hajazitoa. “Siwezi sema kwangu kuna tatizo ni kujipanga tu licha ya changamoto za wezi wa kazi zetu ambao wanatukatisha tamaa,” alisema.
“Lakini nashukuru kuona serikali tayari imeanza kurudisha matumaini kwa kujaribu kuweka sheria ili tupate haki zetu kwa sababu wasanii wengi walikuwa wazito kufanya kazi kwa sababu wanaona hata nikifanya sipati yale mafanikio ambayo nahitaji,” aliongeza.
“Mimi nina movie nyingi nitaanza kuzitoa mwaka 2016 mwanzoni kwa sababu tayari tumeshaanza kuona dalili za kile tunachokihitaji.”
Tags
HABARI ZA WASANII