NIJUZE NIJUZE Author
Title: HARMONIZER KWA NJIA HII ANAYOITUMIA JE ITAMTOA..? AU NDIO ANAPITA ALIPOPITA DIAMOND PLATNUMZ
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Tunajua kuwa Diamond ni msanii mwenye kipaji, anayejituma na nidhamu yake ya kazi inaweza kuhamisha milima, lakini hakuna anayeweza kubi...
Tunajua kuwa Diamond ni msanii mwenye kipaji, anayejituma na nidhamu yake ya kazi inaweza kuhamisha milima, lakini hakuna anayeweza kubisha kuwa uhusiano wake na wasichana maarufu ulimsaidia kumpa jina.

Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Jokate, Zari na wengine ambao hatukuwahi kuthibitisha, wamelijenga zaidi jina lake, na of course, yeye pia amewapa fursa hiyo pia.

Inaonekana kuwa Harmonize anaanza kutumia njia za bosi wake pia kutafuta tobo.

Hivi karibuni muimbaji huyo wa Aiyola amekuwa akiitumia kadi ya ‘mademu’ vyema. Unakumbuka wiki mbili zilizopita alipohojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV na Dullah akamuuliza kama tetesi kuwa ana uhusiano na Rose Ndauka ni za kweli?

Harmo alikanusha japo alikiri kitu kimoja kuwa, ni kweli yeye na muigizaji huyo ni washkaji na kwamba siku moja kabla ya hapo waliwasialiana. Kauli yake haikupokelewa vizuri na Ndauka aliyeiangalia show hiyo. Muigizaji huyo alikanusha kuwa na ushkaji wowote na msanii huyo zaidi ya kuwa karibu na bosi wake Diamond.

Wiki hii pia muimbaji huyo amevuta attention ya watumiaji wa Instagram baada ya video inayomuonesha akipigana mabusu na mrembo Huddah wa Kenya kusambaa. Controversial ni jina la kati la Huddah na hivyo hii ni kadi ambayo Harmo akiitumia atakiki fasta!

Kijana anaendelea kucheza pia na akili za mashabiki kwa mtindo alioutumia bosi wake wa kupost picha akiwa na warembo na caption zenye utata.
Harmonize
“Kura za watu wengi zinasema nikuache uende ingawa kishingo upande sina budi kuwasikiliza mana hawa ndio wanaosababisha niitwe Harmo. Kama uzuri na kasura kako ka upole ulicho kitegesha ili upate poo… umechemka mana mateso niliyo yapata nayajuwa mwenyewe na ndugu zangu waliokuwa wakinifariji kukuthitishia kuwa wewe hufai naomba niulize watu uone wangapi,” ameandika kwenye picha akiwa na msichana mrembo wa SA.

Swali ni je, njia hii itamtoa?

About Author

Advertisement

 
Top