AKUDO IMPACT- TUMEMFUNDISHA MUZIKI CHRISTIAN BELLA

Aliyewahi kuwa meneja wa Akudo Impact Patrick Muyanzi ameeleza kuwa mafanikio ya msanii Christian Bella yanatokana na mchango mkubwa wa mafunzo ya kisanaa aliyoyapata kipindi yupo kwenye bendi hiyo.
Christian BellaKiongozi huyo amesema Akudo Impact ni Band mama ambayo inaongoza nchini Tanzania kwa kutoa wasanii wenye vipaji akiwemo Christian Bella, Tarsisi Masela na kuongeza kuwa mafunzo yanayopatikana Akudo Impact hayapatikani kwenye Band nyingine yeyote.
Akudo Impact
Kwa upande wake mlezi wa Band hiyo ambaye pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri na ubunge katika taifa la Tanzania Profesa Juma Kapuya ameeleza kuwa Akudo wamejipanga na ujio mpya ambao wanaimani utawakonga nyoyo wapenzi wa burudani nchini hivyo waendelee kuwaunga mkono.
Previous Post Next Post