Wema Isaac Sepetu
Maneno kuntu! Staa mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Isaac Sepetu amefungua kinywa chake na kusema kuwa endapo Mgombea wa Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa angeshinda kuwa Rais wa Tanzania katika uchaguzi uliopita, bila hiyana yeye angehama nchi.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Wema alisema kuwa anamshukuru Mungu kuwa anasubiri kwa hamu kuapishwa kwa mshindi wa nafasi hiyo, Dk. John Magufuli ambaye anamuamini ni mchapakazi asiyekuwa na urafiki na mtu mzembe.
“Sifichi, kweli kabisa Lowassa angeshinda, bila ubishi ningehama nchi yangu niipendayo,” alisema Wema.