Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Lipumba amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na kumpongeza kwa hotuba nzuri iliyoweka mwelekeo mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Pia Prof Lipumba amesifu na kuunga mkono Juhudi za Mhe Rais katika kupambana na wakwepa kodi na wahujumu uchumi.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30