Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI MSIFANYE KAMPENI SIKU YA UCHAGUZI - LHRC
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wito huo umetolewa na mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) dawati la uangalizi wa shughuli za serikali Hussein ...
LHRC
Wito huo umetolewa na mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) dawati la uangalizi wa shughuli za serikali Hussein Sengu, alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Super Mix kinachorushwa na East Africa Radio, akitoa elimu kwa wananchi kuhusu vitendo ambavyo havitakiwi siku ya kupiga kura tarehe 25 oktoba mwaka huu.

Sengu amesema mwananchi yeyote hatarusiwa kuvaa au kuwa na kitu ambacho kitaashiria alama ya chama fulani, kwa sababu siku ya uchaguzi hairuhusiwi kufanya kampeni ya aina yoyote.
"Wananchi wafahamu kwamba kanuni na sheria za uchaguzi, zinasema siku hiyo ya kwenda kupiga kura kuanzia asubuhi, haitaruhusiwa mtu yeyote kuvaa au kuwa na kitu ambacho kitaashiria alama ya chama fulani, kuanzia mavazi, bendera, kofia ya chama fulani, haitaruhusiwa kabisa, haitaruhusiwa kwa sababu siku ya uchaguzi hakuna kampeni, kwa hiyo kwa kufanya hivyo utakuwa umekipelekea chama chako kichukuliwe hatua ya kisheria", alisema Sengu.

Pia Sengu amewataka wananchi walioweka bendera za vyama vyao sehemu mbali mbali kujiandaa kutoa bendera hizo siku ya tarehe 24, kwani ndio siku ya mwisho ya kampeni, na chama chochote ambacho kitakiuka kitachukuliwa sheria.
"Na hawa wote wanaobandika bendera zinatakiwa zisiwepo siku ile, kwa hiyo walioweka bajeti kubwa ya kuweka matangazo na vipeperushi, pia wanatakiwa waweke bajeti kubwa kuhakikisha kwamba siku nne zijazo wanatoa kila kitu, kwa sababu mimi naamini kuvitoa ni ghali kuliko kuweka, watu wataanza kusikia uvivu kuvitoa"
, alisema Sengu.

Pamoja na hayo Sengu amewataka wananchi kuwahi mapema na kuangalia majina yao kama yapo kwenye orodha ya wapiga kura, na pia kuwa utu kwa kuwapisha wale wa kwenye makundi maalum akitolea mfano wazee, walemavu na wajawazito kwenye foleni ya kupiga kura.

About Author

Advertisement

 
Top