Unknown Unknown Author
Title: MAJAJI WAPEWA MAFUNZO KUENDESHA KESI ZA UCHAGUZI, SHERIA INASEMA PIGA KURA KAA MITA 200
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Majaji zaidi ya 40 wamepatiwa mafunzo ya namna bora na ya haraka zaidi ya kuendesha kesi za uchaguzi endapo zitajitokeza baada ya uchaguzi ...
Majaji zaidi ya 40 wamepatiwa mafunzo ya namna bora na ya haraka zaidi ya kuendesha kesi za uchaguzi endapo zitajitokeza baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.
Mohammed Chande Othman
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman

Akiongea katika ufunguzi wa mafunzo hayo Jaji mkuu Othman Chande amesema kuwa wamefikia hatua hiyo sababu uchaguzi wa mwaka huu unaonekana kuwa na mihemko mingi na wanatarajia kesi nyingi zinaweza kujitokeza pia.

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume ya uchaguzi jaji Damian Lubuva amepongeza mtandao wa walinzi wa haki za binaadamu kwa kuandaa mafunzi hayo kwani utakuwa msaada mkubwa kwa walalamikaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka endapo watakuwa na malalamiko yoyote.

Pia Jaji Lubuva ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa sheria inawataka wapiga kura kukaa mita mia mbili baada ya kupiga kura na kama kuna mabadiliko yoyote ya sheria hiyo, mahakama ndiyo itakayo amua.

About Author

Advertisement

 
Top