HALIMA Yahya ‘Davina’ amehamasika na mambo ya kisiasa hivyo, kujiandaa kwa kujifua vyema kwa ajili ya msimu ujao wa uchaguzi (2020).
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Davina ambaye ni msanii wa filamu Bongo, alisema kufuatia kupata fursa ya kushiriki kampeni kwa nafasi yake, maeneo mbalimbali ya nchi, amejikuta akishawishika kuwa kiongozi na kwamba baada ya miaka mitano, endapo Mungu atamjaalia uzima, atagombea nafasi ya ubunge, mkoani Iringa.
“Sikuwa na mzuka na mambo ya siasa kabisa lakini kushiriki kwangu kampeni za kumnadi Magufuli maeneo mbalimbali nchini, nimeingiwa na ujasiri wa kujiingiza huko na naamini nitamudu nikijipanga, kikubwa tuombe uzima,” alisema Davina.