Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI WA MKOANI MTWARA WATAKA KAMPENI ZA KISTAARABU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow, Mtwara. Baadhi ya wananchi mjini Mtwara wamewataka wagombea na viongozi wa vyama vya siasa kutangaza sera na ilani za uch...
Na.Ahmad Mmow, Mtwara.
Baadhi ya wananchi mjini Mtwara wamewataka wagombea na viongozi wa vyama vya siasa kutangaza sera na ilani za uchaguzi za vyama vyao badala ya kutukunana na kuchafuana.
Lindiyetu Blog News
Wakizungumza na Lindiyetu.com kwa nyakati tofauti mjini Mtwara. Wananchi hao walisema baada ya kampeni za uchaguzi ujao kuanza, baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vyao, wameanza kuhubiri matusi na kuwachafua wagombea na viongozi wa vyama vingine.

Amina Lupapa(32) mkazi wa Chikongola, alisema baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kampeni kuanza, zimeanza kusikika lugha za matusi na kuchafuana. Alisema hali hiyo isipo zuiawa inaweza kusababisha vurugu na kuhatarisha amani na utulivu ulipo hapa nchini.
"Sisi hatutaki vurughu kwa sababu mwisho wa siku waathirika wakubwa ni akina mama, watoto, vikongwe na walemavu. Sisi watu wa Mtwara tunayajua madhara ya vurugu, hatutaki watupeleke huko," alisema Amina.

Alisema tume ya uchaguzi hainabudi kukemea kwa nguvu vitendo na kauli zinazoashiria uvunjifu wa amani bila kujali nyadhifa na vyeo vya watu wanatenda na kutoa kauli hizo.

Abdallah Mniha(32) wa Magomeni alisema kauli za baadhi ya wagombea, hazifai kwani hazina tija kwa wananchi. Alisema wananchi wanataka kusikia sera na ilani ili wafanye uamuzi sahihi siku ya kupiga kura baada ya kuzisikia ilani na sera za wagombea wote. Alisema hata hivyo baadhi ya wagombea na viongozi wa vyama wameacha kutimiza wajibu huo muhimu na kuanza kutukanana.
"Wajue wanatutukana hata tunaowasikiliza, wagombea na viongozi wanaofanya hivyo watambue kuwa wanajimaliza wenyewe," alisema Abdallah.

Habiba Rashid (28) wa Kihanga alisema katika kipindi hiki cha kampeni, wananchi wanatakiwa kuhudhuria mikutano ya kampeni na kusikiliza vyombo vya habari ili wazisikie ilani za vyama vya na sera za wagombea ili wapate viongozi bora.
"Licha ya kuhudhuria mikutano lakini pia tufuatilie kauli na vitendo vyao, juzi baada ya kuanza kampeni tumeanza kuzisikia lugha zisizo za kiungwana na wengine wanakiuka sheria za tume wanakusanya watu bila kutoa taarifa polisi," alisema Habiba.

Tangu kuanza kampeni za uchaguzi yameendelea kutokea maoni mbalimbali baada ya wagombea wa wanafasi mbalimbali kuanza kunadi sera na ilani za vyama vyao. Huku wengi wao wakipati hofu juu ya hatima ya amani na utulivu uliopo hapa nchini.

About Author

Advertisement

 
Top