Unknown Unknown Author
Title: MGOMBEA UBUNGE KUPITIA CCM ATOA ANGALIZO KUHUSU AHADI ZA WAGOMBEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow, Liwale. Mgombea wa ubunge kupitia CCM katika jimbo la Liwale, Faith Mitambo, amewaasa wanachi kuzipima ahadi za wagombea na...
Na.Ahmad Mmow, Liwale.
Mgombea wa ubunge kupitia CCM katika jimbo la Liwale, Faith Mitambo, amewaasa wanachi kuzipima ahadi za wagombea na viongozi wa vyama vya siasa katika kipindi hiki cha kampeni. Kwani baadhi ya ahadi hazitekelezi na zimejaa ulaghai na uongo.
Lindiyetu Blog News
Mitambo alitoa wito huo jana mjini Liwale kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho wilayani Liwale. Mgombea huyo ambaye anaomba ridhaa kwa mara nyingine baada ya kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mitano iliyopita. 

Alisema baadhi ya wagombea wamekuwa wakitoa ahadi ambazo haziwezi kutekelezeka kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi na zakimataifa. Bila kutaja majina ya viongozi na wagombea waliokwenda kutoa ahadi katika jimbo hilo ambazo hazitekelezeki, alisema baadhi ya wagombea wamehaidi kupitisha barabara kwenye mapori ya hifadhi na mbuga, zilizopo katika jimbo hilo, kiwamo mbuga ya Selous jambo ambalo haliwezi kufanyika kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.
"Yapo ya kikamilifu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika jimbo hilo. Ikiwamo sekta za elimu, mawasiliano, umeme, afya, baraba na maji. "kuhusu suala la vijana na wanawake nilishaanza kulifanyia kazi, katika kipindi kilichopita nilitoa shilingi milioni moja katika kila kijiji kwa ajili ya vikundi vya wanawake" nahaidi kutoa kwa vijana shilingi milioni kumi kila mwaka kutoka kwenye mfuko wa jimbo,"alisema mgombea huyo.

Pia alihadi kwamba iwapo atachaguliwa atahakikisha shule zote za sekondari zilizopo katika jimbo hilo zinafikishiwa umeme wa uhakika. Ambapo katika miaka mitano iliyopita alipeleka katika shule hizo umeme unaotokana na nguvu za jua(sollarpower) ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kikamilifu.
"Vipo vijiji havina mawasiliano ya simu, tatizo hilo limeanza kushugulikiwa. Zipo kampuni zimeahidi kuanza kujenga minara katika baadhi ya vijiji ili huduma hiyo ianze kupatikana,"aliongeza kusema.

Aliwaasa wananchi hao watambue kuwa mbunge ni kiungo baina ya wananchi na serikali yao. Ambapo miongoni mwa majukumu yake nikuwasikiliza, na kupeleka matatizo na mahitaji yao serikalini kwa utekelezaji. Hivyo siyo vema kumuhukumu kwa kutokamilika kwa baadhi ya miradi ya maendeleo kwa wakati. Ambapo imejiwekea taratibu nzuri za namna ya kuyashugulikia.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya wa chama hicho, Abasi Matulilo aliwaomba viongozi na wagombea wanaotokana na chama hicho kufanya kampeni za kistaharabu ambazo zitawafanya wananchi wakiamini wawaamini pamoja na chama chao.
"Epukeni lugha zisizofaa kama matusi na kashfa kwani wapo watu ambao sio wanachama wa CCM wakuwa wanasiliza kampeni zetu,sasa kama mtakuwa na lugha sizizo na ustaharabu hawawezi kutuunga mkono," alisema Matulilo.

Mitambo anachuana na mgombea wa CUF kupitia UKAWA, Zuberi Kuchauka katika nafasi ya ubunge.

About Author

Advertisement

 
Top