Unknown Unknown Author
Title: HII NDIO KAULI YA LINEX BAADA YA KUSAMBAA KWA WIMBO "Because of You" UNAOSEMEKANA NI WAKE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msanii Linex anayefanya vizuri na ngoma ya Salima ft Diamond Platnumz amefunguka juu ya wimbo uliosambaa kwa kasi unaodaiwa kuwa amefanya...
Msanii Linex anayefanya vizuri na ngoma ya Salima ft Diamond Platnumz amefunguka juu ya wimbo uliosambaa kwa kasi unaodaiwa kuwa amefanya na msanii Baraka Da Prince na kupewa jina la "Because of You".
Linex
Sunday Mjeda "Linex"
"hio ngoma nlifanya nkiwa Kahama kwa ajili ya kumsaidia msanii flani ambae anaanza mziki ili apate mwongozo wa jinsi gani ataimba kwenye wimbo wake na nlikuwa na Baraka da Prince"

"So nkaona na yeye aweke sauti yake ili huyu dogo aweze kuelewa atapitaje kwenye ngoma yake maana idea yake ilikuwa kama hii ila akawa hajui namna ya gani ya kupiga vocal nzuri", 

"Nashangaa yule producer kaunga zile vocal ametoa kama wimbo wangu na Baraka na kuupa jina "Because of You", 

"Mimi sijatoa wimbo wowote na hio ngoma sio ndomana hata ukiskiliza ipo chini ya kiwango" alisema Linex.

Sikilia hapo chini Linex Akiongea na Lindiyetu.com kuhusu Ishu ya Wimbo Huu.
 Wimbo wenyewe Huu Hapo chini;

About Author

Advertisement

 
Top