Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Mizengo Pinda akiingia akita Banda la NHIF katika Viwanja vya Ngongo katika Sherehe za Nane nane ambapo Mh. Waziri alikuwa mgeni rasmi na ndio aliyefungua maonyesho hayo yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu wa Tanzania Hapo jana aliweza kufungua maonyesho ya wakulima Nane Nane ambayo kitaifa yanafanyika kwa mara ya Pili mkoani Lindi, pia alipata fursa ya Kulitembelea Banda na Bima ya Afya (NHIF) na kupata maelezo ya Huduma zitolewazo katika Banda hilo za Afya na Ushauri kwa wananchi.
Wananchi wakipata Huuma ya Elimu kuhusiana na Huduma zitolewazo na Mfuko wa Bima ya Afya katika Banda la NHIF lililopo katika Viwanja vya Ngongo katika Sherehe za Nane nane Mkoani Lindi.
Wafanyakazi wa NHIF wanaotoa Huduma katika Viwanja vya Ngongo katika Sherehe za Nanenane Mkoani Lindi.
Burudani nazo hazikosi katika Banda hilo la NHI, Ewe mkazi wa Lindi Unakaribishwa kulitembelea banda hili iliuweze kuelimika na kujua Huduma zitolewazo na Mfuko huu wa Bima ya Afya na Uweze kujiunga ili nawe ufaidike na Mfuko huu. Banda lao liko jirani kabisa na Jukwaa Kuu.