Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania akikata Utepe Kuashiria kufungua rasmi sherehe za Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi, Ufunguzi huo umefanyika Hapo jana katika Viwanja vya Ngongo/Tulieni Mkoani Hapa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliweza Kutembelea Mabanda yaliyopo katika Viwanja hivyo na hapa alikuwa katika Banda la Benki ya CRDB akipata maelekezo ya huduma zitolewazo na Benki hiyo Ndani ya Viwanja hivyo vya Nane Nane Mkoani Lindi. Agosti 4, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mashine ya kunyonyoa kuku wakati alipotembelea banda la kampuni ya ubia kati ya watanzania na wachina ya Poly Machinery ya Millennium Busibess Park jijijni Dares salaam, baada ya kufungua maonyesho ya Nanenane kwenye uwanja wa Ngongo Lindi Agosti 4, 2015.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusiana na jinsi ya kuziharibu Pesa zilizochakaakutoka kwa Afisa wa Benki kuu wakati alipotembelea Banda lao lililopo katika Viwanja vya Nane nane Mkoani lindi wakati wa Uzinduzi wa Maonyesho hayo agost 4,2015
Akiwa katika Banda la Mfuko wa Bima ya Afya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliweza pata maelekezo ya Huduma zitolewazo na Mfuko huo katika viwanja hivyo vya Nane nane agost 4, 2015.