Bi. Gaudensia Simwanza ambaye ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Kutoka TFDA akiweka sawa Vipeperushi na Majarida maalumu kwa ajili ya Utoaji Elimu kwa wananchi juu ya Matumizi sahihi ya Madawa na Vipodozi vitumiwavyo na Binadamu na Madhara yake...Hayo yote unayapata katika Banda lao lililopo katika viwanja vya Nane Nane Ngongo Lindi karibu Kabisa na Banda la Bima ya Afya.
James Ndege ambaye ni Afisa Mwandamizi Uelimishaji Jamii kutoka TFDA nae yupo kwa ajili ya Kukuhudumia wewe Mkazi wa Lindi kuhusiana na Madawa mbalimbali yanayotumiwa na Binadamu kwa ajili ya chakula pamoja na Vidpodozi kwa ajili ya Urembo. Je unajua ni Vipodozi gani Vimepigwa Marufuku? Fika katika Banda lao upate kujua Hakika utapata manufaa makubwa.
Kama anavyoonekana Bi. Gaudensia Simwanza akitoa huduma ya Ushauri kuhusiana na Madawa mbalimbali yanayotumiwa na Binadamu kwa Mwananchi aliyeweza kufika katika banda lao lililopo katika viwanja vya Nane nane karibu kabisa na Banda la Bima ya Afya
Bi Gaudensia Simwanza kutoka mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) akimweleza mwanchi ni jinsi gani Vipodozi vilivyopigwa marufuku kutumika kwa binadamu vinavyoweza kuathiri ngozi yake. kushoto ni Vipodozi vilivyopigwa marufuku kutumika hapa nchini na mamlaka hiyo. Hivyo ndugu Msomaji Unashauriwa kufika katika banda lao ilikujua Je nawewe upokatika Hatari ya Kuharibu Ngozi yako?
Nae mwana Habari Abdulaziz alikuwa miongoni mwa watembeleaji wa Banda hilo na hapa alikuwa akipata maelekezo kutoka kwa Maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa YFDA.