Prof. Ibrahim H. Lipumba
CHAMA CHA WANANCHI CUF.
KUNG’ATUKA WADHIFA WA MWENYEKITI WATAIFA CUF.
(HOTUBA YA PROF. LIPUMBA KUJIUZURU UENYEKITI CUF TAIFA).
Kwa mara ya kwanza nilichaguliwa na mkutano mkuu wa CUF kuwa mwenyekiti wa Taifa wa Chama November 1999, nilichaguliwatena kushika wadhifa huu 2004,2009 na 2014.
Nimejitahidi kukijenga chama chetu hasa Tanzania Bara, ndani ya chama na nje ya chama, nimejitahidi kujenga umoja katiyawazanzibari na wananchi wa Tanzania Bara. January 25 2001, nilikamatwa na polisi, kupigwa na kuvunjwa mkono, kuporwa saa nakuwekwa jela kwa kudai Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, Utawala bora na uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2000 urejewe iliwazanzibari watendewe haki na wachague viongozi wanaowataka.
January 27 2015 Chama kiliandaa niongoze maandamano na mkutano wa hadhara kuomboleza mauaji yaliyofanywa na vyombovya dolaZanzibar na hasa Pemba tarehe 27January 2001. Polisi walizuia maandamano hayo na kutupa taarifa tarehe 26 Januarysaa 12:30 jioni. Nilipoenda kuwapa taarifa wanachama na wananchi waliokusanyika kufanya maandamano, mimi na viongozi nawanachama wa CUF wa Tanzania Bara tulikamatwa, kupigwa na wengine kuumizwa vibaya. Hivi sasa tumebambikiziwa kesi nakushitakiwa kwa kula njama kufanya vitendo vya uhalifu na kufanya maandamano yasiyo halali. Kesi iliyoanza tarehe 29 January 2015 bado inaendelea mahakama ya kisutu.
Sikuwa na nia ya kugombea uenyekiti mwaka 2014, lakini mchakato wakupata katiba iliyotokana na maoni ya Wananchi ilinisukumaniendelee na uongozi wa CUF.
Rasimu ya Katiba ya Tume ya mabadiliko ya Katiba ilikuwa na mambo ya msingi ambayo kama tungefika muafaka wa kitaifakuhusu katiba hiyo tungeweza kuanza kuifua Tanzania mpya inayoenzi na kuzingatia Tunu za Taifa zautu,uzalendo,uadilifu,umoja,uwazi na uwajibikaji.
Ndani ya bunge maalum la katiba tulianzisha Umoj wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwalengo la kutetea nakuyaheshimu maoniyawananchi yaliyoratibiwana Tume ya JajiWarioba na kuwekwa katika Rasimu ya Katiba. Tumeendeleza kushirikiana ndni ya UKAWAkuelekea kwenye uchaguzi mkuu ili hatimaye tupate katiba mpya inayotokana na maoniya wananchi natuwena serikali itakayoenzina kuyatekeleza yaliyomondani ya katiba hiyo.
Katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi ni nyenzo ya kufikia malengo mapana zaidi ya kuwa na Taifa la wananchiwalioelimika na kujitambua,wenye afya bora,linalojenga uchumi imara unaoongeza ajira kwa vijana wetu, kutokomeza umasikini,kutumia rasilimali na maliasili za nchi kwa manufaa ya wananchi wote, kupambana na rushwa na ufisadi na kuwa na taifa lenyeutu,uzalendo,uadilifu,umoja, uwazi na uwajibikaji.Katiba mpya inayosimamiwa na wananchi itaiwajibisha serikali kutenda haki sawakwa wote.
Nimeshiriki katikavikaovingi vya UKAWA vilivyotufikisha hapa. Hata hivyo Dhamira na nafsi yanguinanisuta kuwa katika maamuziyetu ya UKAWA tumeshindwa kuenzina kuzingatia tunu za Taifa , utu,uzalendo,uadilifu,umoja na uwajibikaji. Rasimu ya Katiba namaudhui yake tumeyaweka kando.
Walioipinga Rasimu ya katiba ya Wananchi ndani ya Bunge maalum la Katiba ndiyo tunaamini wataturahisishia kushinda uchaguzi.Tumeshindwa kuongozwa na maadili.
Tarehe 1 August 2015 niliiarifu Kamati ya utendaji ya Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu wa chama chetu kuwa nitawajibika nakujizulu uenyekiti wa Taifa baada ya wenzangu kukamilisha taratibu za ushirikiano ndani ya UKAWA.
Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Juma Duni Haji ambaye Baraza Kuu lilimpitisha kuwa Mgombea wa uwakilishi jimbo la Bububu amehama chama na kujiunga CHADEMA na kuteuliwa kuwa Mgombea mwenza wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu waoktoba 2015.
Leo hii nimeikabidhi Ofisi ya Katibu Mkuu , barua yangu ya Kung’atuka nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, lakini naendelea kuwamwanachama wa CUF na kadi yangu imelipiwa mpaka mwaka 2020.
Katika kipindi cha kabla ya uchaguzi mkuu nitajishughulisha na kuandaa ushauri wa mambo yanayopaswa kufanywa na serikaliijayo ikiwa ni pamoja na:-
- Kujenga uchumi imara unaoongeza ajira kwavijana wetu
- Kuhakikisha kila mama wajawazito na watoto wanapata lishe bora ili watoto wajenge ubongo na maungo yao yawe na wawe nakinga ya mwili.
- Tanzania inahitaji mapinduzi ya kilimo kuongeza uzalishaji wa chakula na mazao mengine ya biashara.
- Mkakati madhubuti wa kuboresha elimu ili tuwe na Taifa la wananchi walioelimika na wabunifu wanaoweza kuajirika nakujiajiri.
- Kuweka utaratibu wa uboreshaji wa huduma za kinga na tiba ya Afya na kuanza kujenga mfumo wa huduma za afya uliokamilikatoka zahanati hadi hospitali za rufaa.
- Kujenga mfumo madhubuti wahifadhi ya jamiihasa kwawazee ambao hutelekezwa na kutopata matunzo kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki kwa sababu na wao ni masikini.
- Kusimamia ujenzi wa miundombinu mizuri kama vile barabara, reli, bandari,viwanja vya ndege,nguvu za umeme,mawasilianonamaji. Miundombinu inayounganisha nchi jirani ni muhimu kwakukuza uchumi na ulinzi wataifa.
- Kuongeza ukusanyajiwa mapatoya serikalikufikia asilimia 20 ya pato la taifa na kuhakikisha matumizi ya serikali yana tija.
- Rushwa ni aduiwa haki na ni adui wa maendeleo. Rushwa na ufisadi ni mfumo wa utendaji ndaniya serikali .hata hivyo mkakatiwa kupambana na rushwa unahitaji utashi wa kisiasa

- Kuweka mkakati wa kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals) nchini Tanzania .
Baada ya uchaguzi nitajikita katika kufanya utafiti na kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya uchumi shirikishi wa Taifa letu.
Nawashukuru wanachama wa CUF na wananchi kwa ujumla kwakuniunga mkono wakati nikiwa kiongozi wa chama hiki. Nawaomba radhi sana wanachama na wananchi walioniamini na kuonyesha mapenzi makubwa kwangu na katika uongozi wangu. Katika hali halisi iliyopo ndani ya uongozi wa chama chetu mimi naonekana ni kikwazo na kwa hiyo siwezi kuwanamchango wamaana kama Mwenyekiti katika mapambano ya kudai haki sawa kwa wote katika kipindi hili.
HAKI SAWA KWA WOTE

PROF. IBRAHIM HARUNA LIPUMBA,
Mwenyekiti Mstaafu wa CUF,
06 Agosti 2015.