Bechi la Ufundi la timu ya Wailes City katika mchezi wao wa Fainali dhidi ya Stend Worious, mchezo uliofanyika uwanja wa Ilulu Lindi.
Bechi la Ufundi la timu ya Stend Worious katika mchezi wao wa Fainali dhidi ya Wailes City, mchezo uliofanyika uwanja wa Ilulu Lindi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu (TFF-LINDI, mwenye Suti) Suitbert Milanzi akipeana mikono na Mdhamini wa Mashindano ya Mgumia Cup Ndg Hassani Kaunje ambaye ni mtia nia wa Nafasi ya Ubunge Jimbo la Lindi kupitia tiketi ya CCM
Leo ikiwa ni fainali ya Ligi ya Mgumia Cup Mkoani Lindi ambayo ilikuwa imethaminiwa na Hassani Kaunje Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM ambaye ni Mtia nia wa Nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Lindi, Imefikia tamati kwa kuikutanisha Timu za Mjini Lindi Wailes City na Stendi Worious ambapo Wailes City waliweza Kuibuka Kidedea kwa kuifunga Stendi Worious kwa jumla ya Magoli 3 - 1.
Ni Msafiri Kaambwili ndio aliepeleka kilio kwa Timu ya Stend Worious wenye maskani yao Stendi Kuu ya Mabasi Mkoani hapa kwa kuifungia timu yake ya Wailes City magoli yote Matatu ambapo magoli hayo yote aliweza kuyafunga katika kipindi cha kwanza cha Mchezo huo ikiwa ni dakika ya 28, 31 na 44. Ambapo bao pekee la kufutia machozi la Stendi lilifungwa na Mchezaji Anaafi Seleman mnamo dakika ya 50 kipindi cha pili.
Kufuatia Ushindi huo wa Goli 3 -1 Wailes City wakatawazwa kuwa washindi wa michuano hiyo na kupata dhawadi ya Pesa tasilimu kiasi cha Tsh 400,000.00 (laki nne tu) pamoja na Mpira mpya mmoja, huku timu ya pili ya Stendi ikisalia na Kitita cha Tsh 300,000.00 (Laki tatu tu) na Mpira mpya mmoja kwa kushika nafasi hiyo ya pili. Nafasi ya Tatu ilichukuliwa na Timu ya Muunngano kutoka katika kata ya Mingoyo iliyopo nje kidogo ya mji wa Lindi na kupewa dhawadi ya Tsh 200,000.00 (laki mbili tu) na Mpira mpya Mmoja.
Nahodha wa Timu ya Mawasiliano akikabidhiwa zawadi ya Mshindi wa Tatu wa Mashindano ya Mgumia Cup na Mgeni rasmi Hassani Kaunje leo hii katika viwanja vya Ilulu.
Nahodha wa Timu ya Stendi akikabidhiwa zawadi ya Mshindi wa Pili wa Mashindano ya Mgumia Cup na Mgeni rasmi Hassani Kaunje leo hii katika viwanja vya Ilulu.
Nahodha wa Timu ya Wailes City akikabidhiwa zawadi ya Mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Mgumia Cup na Mgeni rasmi Hassani Kaunje leo hii katika viwanja vya Ilulu.
Mashabiki wa Mpira wa Miguu walioweza kujitokeza kushuhudia Fainali ya Mashindano ya Mgumia Cup yaliyofanyika Mkoani Lindi leo hii katika Uwanja wa Ilulu na Wailes City Kuibuka bingwa wa Mashindano hayo.
Mashabikiwa wa Wailes City wakishangilia Ushindi Baada ya Mpira kumalizika na kuibuka Bingwa kwa kuifunga timu ya Stendi kwa Jumla ya Magoli 3-1.