Hapo jana Mchezaji aliesajiliwa kwa ada kubwa kuwahikutokea klabuni hapo kwa msimu uliopita kutoka Real Madrid Angel Di Maria alishindwa kuungana na Timu yake iliyopo Marekani.
Kocha Mkuu wa Manchester United Luis Van Gaal ameshangazwa na Kitendo hicho cha Mchezaji huyo wa Taifa la Argentina kugoma kuungana na wenzake katika Tour ya Timu hiyo Nchini Marekani, Di Maria alitakiwa kupanda ndege na kuungana na timu yake kwa ajili ya Mchezo wao na Barcelona lakini haikuwa hivyo na kocha huyo ameshindwa kuelewa ni kwanini ameshindwa kutekeleza agizo hilo.
Klabu ya PSG imeweka dau la Paundi milioni 46.5 ilikumnunua Mchezaji huyo ambaye anaonyesha kutokuwa na furaha Oldtraford na wanategemea Dili hilo linaweza kukamilika siku ya Jumatatu.