Unknown Unknown Author
Title: CHADEMA NACHINGWEA WAPATA MGOMBEA UBUNGE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow,Lindi. Wakati Chama Cha Mapinduzi wilayani Nachingwea, mkoani Lindi kikiendelea mchakato wa kampeni za kura za maoni ili k...
Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Wakati Chama Cha Mapinduzi wilayani Nachingwea, mkoani Lindi kikiendelea mchakato wa kampeni za kura za maoni ili kumpata mwanachama wa chama hicho atayepeperusha bendara ili awemgombea wa ubunge katika jimbo la Nachingwea.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)
(Picha kutoka Maktaba)
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kimepata mgombea atayekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao katika nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Katika uchaguzi uliofanyika juzi katika ukumbi wa Nachengwea Resort(NR)mjini Nachingwea, Wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya wa chama hicho walimchagua Dkt Mahadhi Mmoto, kuwa mgombea wake wa ubunge katika jimbo la Nachingwea, ambalo kabla ya bunge kuvunjwa lilikuwa linawakilishwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mathias Chikawe.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliohudhuriwa na wajumbe 342, mratibu wa kanda ya kusini wa chama hicho, Filbert Ngatunga alimtangaza Dkt Mmoto kuwa ndiye mshindi, baada ya kupata kura 227.

Katika uchaguzi huo kwa mujibu wa maelezo ya Ngatunga, wagombea walikuwa wanne. Ambao ni Dkt Mmoto,Thomas Mmuni aliyepata kura 99, Nurdin Mchora kura 28 na Ramdhani Chimbanga kura 6. Wakati huo huo, chama hicho katika jimbo la Mtwara mjini kilimchagua Joel Nanauka kuwa mgombea wake katika jimbo la Mtwara. Kwamujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Hamisi Namangaya, Mnanauka alipata kura 105 kati ya 179. Nakuwashinda wagombea wenzake watatu, Mohamed Mandoa, Hassan Hanga na Dunstan Mulokozi.

About Author

Advertisement

 
Top