Muda mfupi uliopita Mwanasiasa maarufu nchini Zitto Zubery Kabwe ameweza kutoa tamko la Chama chake kipya cha ACT-WAZALENDO.
Mh. Zitto ameweza kuweka wazi kuwa wao watamsimamisha Mgombea wao kwa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Ujao na tarehe 10/8/2015 wataweza kumtangaza mgombea wao wa nafasi hiyo ya Urais kupitia chama cha Act-Wazalendo.
Zitto ameandika haya katika Ukurasa wake wa Facebook.:
Zitto Kabwe (picha kutoka Maktaba)
Zitto amesema kuwa hawata weza kujiunga tena na Muungano wa vyama vya upinzani nchini ujulikanao kama UKAWA kwa kuwa tangu walivyoweza kupeleka maombi yao mwezi wa nne mwaka 2015, hawajapata Jibu lolote japo amesema kuwa wao wameweza kupokea taarifa zinazosema kuwa kuna chama kimoja wapo kinachounda UKAWA kuwa hakiwataki ACT-WAZALENDO katika umoja huo japo hakuweza kukitaja moja kwa moja ni Chama gani hicho.Mh. Zitto ameweza kuweka wazi kuwa wao watamsimamisha Mgombea wao kwa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Ujao na tarehe 10/8/2015 wataweza kumtangaza mgombea wao wa nafasi hiyo ya Urais kupitia chama cha Act-Wazalendo.
Zitto ameandika haya katika Ukurasa wake wa Facebook.: