
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeteua Naibu Mtendaji Mkuu wa kituo cha Azam Media Group, Tido Mhando kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Soka nchini (FDF).
Katika hatua nyingine Deogratius Lyatto ameteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti na Wajumbe ni Ephraim Mafuru, Beatrice Singano, Joseph Kahama, Ayoub Chamshama wakati Henry Tandau atakuwa Katibu mtendaji wa mfuko huo.Uteuzi huo umefanyika leo katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichoitishwa na Rais wa shirikisho la soka Jamal Malinzi.
Aidha, kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, Kamati ya Utendaji kwa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.
Article Source: Mwanaharakati Mzalendo
Tags
SPORTS NEWS