MSHALE WA MLIMA ILULU:: KWAMWENENDO HUU MAKUNDI YA WAWANIA URAIS YATAENDELEA KUKIJERUHI CHAMA CHA MAPINDUZI.

Wagombea Urais 2015 kutoka CCMWATANGAZA NIA YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUPITIA CCM, 2015

Na. Ahmad Mmow - LINDI.
"Uzee dawa" na msemo huu wawahenga unaonesha jinsi wazee walivyo na thamani inayotokana na umuhimu walio nao katika jamii kiasi cha kufananishwa na dawa. Dawa kazi yake ni kutibu maradhi, kwamba uzee nitiba kwa maradhi lakini siyo ya mwili. Bali migogoro na mitafaruku mbalimbali nk.

Kwani mambo hayo yanapoikumba jamii, taasisi, kampuni nk ni sawa na kupatwa na maradhi. Kwa mtazamo wa wahenga ni kwamba uzee ni miongoni mwa dawa zinazoweza kutibu maradhi ya aina hiyo. Hata hivyo inawezekana kuwa kwa makusudi maalum au kupitiwa, baadhi ya wazee wanashindwa kutambua thamani ya uzee kiasi cha kuukataa kwa kauli zao, na baadhi kwa maitendo yao. Miongoni mwa wazee katika Chama Cha Mapinduzi ambao niliwakubali na kuwaona ndio dawa mujarabu wa maradhi niliyotangulia kuya eleza ni mzee Kingunge Ngombale Mwiru. 

Mzee Kingunge, kwangu ni alama ya Chama Cha Mapinduzi asilia zilizobaki kwa sasa. Kada huyu wa CCM ni miongoni mwa makada wa chache ambao wanatazamwa kama ndio warithi sahihi wa akina hayati mwalimu Nyerere ndani ya chama hicho. Lakini sio ndani ya Chama peke yake bali hata kwa serikali ni miongoni mwa watu wanaoweza kuishauri vizuri kwa maslahi mapana ya taifa.

Anaouwezo huo kutokana na kuhudumu kwa muda mrefu na kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ndani ya serikali. Kutokana na sifa njema, busara na hekima serikalini na kuhudumu kwa muda mrefu. Huku vijiweni viongozi wenye nyazifa kubwa wanaitwa Vingunge. Hata hivyo baba yangu huyu kwa kabila pamoja na kuendelea kuonekana bado hajachoka kifkra, lakini ni kama ameanza kupotea njia na kuukataa uzee kiaina.

Nikutokana na kushiriki na kauli alizotoa kwenye hafla ya kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea urasi mzee wangu mpambanaji mahiri mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia na kukitetea anachoamini. Mtu ambaye hana chembe ya shaka anapoamua kusimamia na kufuatilia jambo, ndugu Edward Lowassa.
Lowasa na Kingunge
Hizo ni miongoni mwa sifa alizonazo jamani, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! Mzee Kingunge pamoja na kuonesha kumuunga mkono mbunge huyo wa Monduli, lakini alitumia fursa hiyo kutoa rai ambayo kwakweli kama ingetolewa kwa wakati na eneo muhafaka ingeendelea kumjenga sana.

Hata hivyo napata mashaka kwamba ameitoa katika wakati na eneo sio muhafaka kabisa. Mzee Kingunge ametoa rai kwa wawania urais na makundi yanayo waunga mkono kumaliza tofauti zao kwa maslahi ya chama na wao wenyewe. Kada huyu alibainisha wazi kuwa hali ndani ya chama hicho sio shwari. Walau tumepata faida ya kujua hilo ambalo hakuna kiongozi yeyote wa chama hicho amewahi kutamka hadharani kwamba ndani ya CCM kunamvurugano unaotokana na tamaa ya urais. 

Badala yake kulikuwa na minong'ono iliyokuwa inatokana na kupigana vijembe baina ya wanao waunga mkono wawania nafasi hiyo ya juu ya uongozi. Mzee Kingunge anawaasa wamalize kwa kufanya vikao vya upatanishi kwa kuwatumia wazee waliondani ya chama hicho pindi wa kiona inafaa kufanya hivyo, au hata wenyewe bila kuwatumia wazee. Hakika rai hiyo hata mimi naikubali kabisa, maana mvurugano huo unatishia uimara wa chama. 

Nakumbuka hayati baba wa taifa alisema bila CCM imara, nchi itayumba. Tena chama legelege huzaa serikali legelege. Hata hivyo mgogoro wangu na baba ni wapi ametolea rai hiyo na wakati gani? Nimeeleza kuwa mzee Kingunge ni kama alama ya CCM na mrithi wa mwalimu kwakuwa na uwezo wa kukemea, kushauri na kuonya kwa maslahi ya chama na nchi kwa jumla.

Hivyo alisitahili kujiweka pembeni katika hatua hizi ya mwanzo wakati wanawe wanatangaza nia ya kugombea, kuchukua fomu, kutafuta wadhamini nk. Hadi pale atakapopatikana mwanachama mmoja atakayepeperusha bendera ya chama hicho. Angejiweka kando na wawania urais wote huku akikemea na kutoa ushauri wa jumla pale ambapo angeona ni muhimu kufanya hivyo. Wala isingekuwa dhambi kumpigia debe na hata pipa mwanachama ambaye atateuliwa na Chama Cha Mapinduzi. Maana yeye ni mwanachama na kada wa chama hicho.

Lakini kwa kuonesha dhahiri anamuunga mkono nani na wakati huo anatoa rai ya kutaka maridhiano baina ya pande zinazohasimiana, haeleweki na kwahakika mimi simuelewi kabisa. Kwangu mimi rai hiyo naiona kama ametoa wito kwa wawania urais wengine wakajisalimishe kwa yule ambaye anamuona anatosha kuwa rais na atakayekuwa rais wa tano wa nchi hii.

Hapo baba yangu amechemka. Labda kama atakwenda katika kila hafla ya mtangaza nia nakutoa rai hiyo na bila kusita kumwagia sifa za kufaa kuwa rais kila mtangaza nia. Hapo sijui kama wenye ubongo unaochemka kama watamuelewa, zaidi ya kuonekana kituko. Kwa kuonesha dhahiri anamuunga mkono mhesheshimiwa Lowassa hakustahili kutoa rai ile pale na wakati ule.

Kwani kwa kitendo kile amejiondoa kuwa ni mzee wa wote bali wa Lowassa katika harakati hizo. Sidhani kama wengine wanaweza kumuamini na kumuomba ushauri sasa kuhusu harakati zao. Ameukana uzee katika chama ameukubali uzee kwa mgombea urais.

Ningekuwa mimi ndiyo Kingunge ningesubiri hadi Lowassa ashinde baada ya kumpigania ashinde, ndipo nikakaa nae nakumtaka awaite mahasimu wake ili waondoe tofauti zao. Nahata kumuomba asiwe na hasira nao na ikiwezekana awaite kwenye uongozi wake ili afanye nao kazi kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa jumla. 

Lakini yote hayo mzee Kingunge ameshindwa kuyakumbuka. Kwa jumla mzee Kingunge ameongeza na kujitia katikati ya mvurugano na mnyukano alioueleza. Sasa kama hali ndiyo hiyo makundi hayo ya urais yatakomaje zaidi ya kuendelea kukitesa Chama Cha Mapinduzi? Waliotegemewa kuwa watakinusuru kupitia busara zinazotokana na uzee ndio hao wanaimba kizee wanacheza kama vijana. Uenda wamekichoka na wanawasaidia wapinzani kukiondoa madarakani. 

Kama ndivyo yatatatimia kwani juhudi za kukisambaratisha naziona ni kubwa kuliko za kukiimarisha. Kama nadanganya, tusubiri tuone kwani siku hazigandi.
Previous Post Next Post