CANNAVARO AMPIGIA DEBE MWINYI MGWALI KUSAJILIWA NA YANGA SC

Nadir Haroub ‘Cannavaro
Wilbert Molandi, Dar es Salaam.NAHODHA na beki kisiki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amewaambia viongozi wa timu hiyo kuwa, kama kweli wanataka beki wa kati, basi wamsajili Mwinyi Mgwali anayekipiga KMKM ya Zanzibar.Yanga hivi sasa ipo kwenye skauti ya kumtafuta beki wa kati mwenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kujiimarisha na Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika mwakani.

Wakati wakisaka beki wa kati, majina ya Mgwali na Salim Mbonde anayeichezea Mtibwa Sugar yametajwa. Mabeki hao wote wapo kwenye timu ya Taifa Stars iliyopo Afrika Kusini ikishiriki michuano ya Cosafa.

Akizungumza na Championi Jumatano, Cannavaro alisema kuwa kati ya vitu ambavyo Yanga watamfurahisha wakivifanya kwenye usajili wa msimu ujao, basi ni kufanikisha usajili wa beki huyo.“Ninasikia Yanga wameanza mazungumzo na Mwinyi kwa ajili ya kumsaji kwenye usajili wa msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa. Sina uhakika na taarifa hizo. “Kama kweli wameanza naye mazungumzo kwa ajili ya kumsajili, basi wasimuache kutokana na uwezo wake, pia uzoefu alionao.“Mwinyi ni mchezaji ninayefahamu uwezo wake ndani ya uwanja, kiukweli kama viongozi wakifanikiwa kumsajili, basi kocha hatakuwa na hofu kama ikitokea siku mimi au Yondani mmoja wetu akaumia kutokana na kuwepo mbadala wetu,” alisema Cannavaro.
>>Champion Magazine
Previous Post Next Post