AZAM KUFANYA USAJILI MPYA KWA NAFASI HIZI TATU, WACHEZAJI WA KIMATAIFA BADO NI UTATA

Azam FC
Khadija Mngwai, Dar es Salaam
TIMU ya Azam FC imefunguka kuwa kocha mpya atakayesaini timu hiyo, atalazimika kufanya usajili wa wachezaji watatu wa timu za Ligi Kuu Bara kwa lengo la kuimarisha kikosi chao katika nafasi ya beki, kiungo na mshambuliaji.

Azam ambayo imemaliza katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi, inahitaji kujiimarisha zaidi katika nafasi hizo tatu ili kuweza kuleta ushindani wa hali ya juu na kufanikiwa kuwa na kikosi bora msimu ujao.Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu wa Azam FC, Idrissa Nassor, amefunguka kuwa kocha mpya atalazimika kusajili wachezaji watatu kulingana na ripoti ya Kocha George Nsimbe.

“Azam tunahitaji kusajili wachezaji watatu safu ya ushambuliaji, beki pamoja na kiungo mmoja ili kuweza kuimarisha kikosi, kuna baadhi ya wachezaji ambao tunafanya nao mazungumzo na yakikamilika tutawaweka wazi. “Suala la wachezaji wa kimataifa bado linatutatiza kwa kuwa tayari tuna wachezaji watano ambao ndiyo idadi inayotakiwa na TFF, hivyo bado hatujajua kama tutaongeza mchezaji mwingine wa kimataifa ama la kwani dirisha bado halijafunguliwa,” alisema Nassor.
>>Championa Magazine
Previous Post Next Post