Haruna Niyonzima (kushoto), Simon Msuva (kulia) na Kpah Sherman wakishangilia baada ya Simon Msuva kuipatia timu hiyo bao la pili.
Mshambuliaji wa Yanga, Kpah Sherman, akishangilia bao aliloifungia timu yake dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa. Yanga imeshinda 5-0. (Picha na Francis Dande).
Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwatoka wachezaji wa Ruvu Shooting.
Na. Mwandishi WetuVINARA wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, Leo hii wameonyesha dhamira thabiti ya Ubingwa kwa kuitandika Ruvu Shooting Bao 5-0 na kupaa kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Azam FC.Ikiwa Azama FC kesho Jumamosi watafungwa na Stand United basi moja kwa moja Ubingwa unaenda Jangwani na hata wakishinda ikiwa Jumatatu Yanga wataichapa Polisi Moro Uwanja wa Taifa Dar es Salaam basi Ubingwa upo Jangwani.
Kwenye Mechi ya Leo, Yanga walikuwa mbele 3-0 hadi Haftaimu kwa Bao za Simon Msuva, Bao 2, na Kpar Sherman.
Kipindi cha Pili Amisi Tambwe aliipa Yanga Bao la 4 na Kpar Sherman kupiga Bao la 5.Azam FC Jumamosi wanacheza Nyumbani kwao na Stand United na ili kuweka uhai matumaini yao finyu ya kutetea Taji watalazimika kushinda tu kitu ambacho pia kitawasaidia kuikwepa Simba ambao wako nyuma yao na wanacheza Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Ndanda FC.
RATIBA::LIGI KUU VODACOMJumamosi Aprili 25Mbeya City v Kagera CitySimba v Ndanda FCAzam FC v Stand United