Unknown Unknown Author
Title: YANGA NA ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA NGOMA NZITO UWANJA WA TAIFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Leo hii huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga walishindwa kuutumia vyema Uwanja wa Nyumbani walipolazimishwa Sare ya Bao 1-1 na ...
Leo hii huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga walishindwa kuutumia vyema Uwanja wa Nyumbani walipolazimishwa Sare ya Bao 1-1 na Klabu ya Tunisia Etoile du Sahel katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Young Africans Sport Club Vs Etoile Du Sahel

Yanga walianza vizuri mno kwa kupata Penati ya Dakika ya Kwanza tu baada ya Kipa wa Etoile du Sahel kumwangusha Simon Msuva na Kepteni Nadir Haroub Cannavaro kufunga Penati hiyo.

Lakini kadri Mechi ilivyoendelea, pengo la Salum Telela lilionekana na Watunisia hao kutawala kabisa Kiungo ingawa hadi Mapumziko Yanga walikuwa mbele 1-0.

Yanga walifanya mabadiliko Kipindi cha Pili kwa kumtoa Kepteni Nadir Haroub 'Cannavaro' alieumia na kumwingiza Salum Makapu.

Etoile du Sahel walisawazisha katika Dakika ya 47 kwa Bao la Mohamed Amine Ben Amor na kuanza staili ya kupoteza muda kulinda Sare yao ya Bao la Ugenini.
Young Africans Sport Club Vs Etoile Du Sahel
Hadii mwisho, Yanga 1 Etoile duSahel 1.

Mechi hii ilichezeshwa na Refa kutoka Msumbiji, Samwel Chirindza, aliesaidiwa na Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe na Jose Maria Bachide wakati Kamisaa ni kutoka Sudan, Salah Ahmed Mohamed.

Yanga itarudiana na Etoile du Sahel huko Tunisia Wikiendi ya Mei 5 wakihitaji ushindi au Sare ya kuanzia Bao 2-2 ili kufuzu.
Young Africans Sport Club Vs Etoile Du Sahel

CAF KOMBE LA SHIRIKSHO ::Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Aprili 17
Association Sportive Olympique de Chlef 1 - 1 Club Africain
Djoliba AC 1 - 2 Hearts of Oak

Jumamosi Aprili 18
Young Africans 1-1 E.S. Sahel 1
Royal Leopards v AS Vita Club
Warri Wolves v Etanchéité
Jumapili Aprili 19
CF Mounana v Orlando Pirates
Al Zamalek v Fath Union Sport de Rabat
Onze Createurs v ASEC Mimosas Abidjan

Young Africans Sport Club Vs Etoile Du Sahel

**Marudiano Wikiendi ya Mei 5
**Washindi 8 wa Raundi hii watajumuika na Timu 8 zilizobwagwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kuwekwa kwenye Droo maalum kupanga Mechi 8 za Mtoano na Washindi wake 8 kutinga hatua ya Makundi ambayo yatakuwa na Makundi mawili ya Timu 4 kila mmoja yatakayocheza Mtindo wa Ligi wa Nyumbani na Ugenini.

About Author

Advertisement

 
Top