Unknown Unknown Author
Title: LIGI KUU VODACOM: SIMBA HOI SOKOINE KWA MBEYA CITY, AZAM YAIPIGA KAGERA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, AzamFC, Leo hii wakiwa kwao Azam Complex, Chamazi, wamefuta balaa ya Sare zilizowaandama na kuichap...
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, AzamFC, Leo hii wakiwa kwao Azam Complex, Chamazi, wamefuta balaa ya Sare zilizowaandama na kuichapa Kagera Sugar Bao 2-1.
Lig Kuu ya Vodacom Tanzania
Ushindi huu umewasogeza Azam FC na kuwakaribia Vinara wa Ligi, Yanga, na sasa wapo Pointi 4 nyuma yao lakini wao wamecheza Mechi moja zaidi.

Mabao katika Mechi hiyo yalifungwa na Frank Domayo kwa Azam FC katika Dakika ya 40 na Kagera Sugar kusawazisha Dakika ya 54 kwa Bao la Babu Ally lakini Gaudence Mwaikimba akaipa ushindi Azam FC kwa Bao lake la Dakika za lala salama.

Huko Morogoro, Polisi Moro waliichapa Ndanda FC Bao 2-0 kwa Bao za Edward Christopher, Dakika ya 64, na Said Bahanuzi, Dakika ya 74.

Huko Sokoine, Mbeya, Wenyeji Mbeya City waliitwanga Simba Bao 2-0 kwa Bao za Paul Nonga katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza na la pili kufungwa na Peter Mwalyanzi katika Dakika ya 69.

Kesho Jumapili ipo Mechi moja tu ya Ligi huko Mabatini, Mlandizi kwa Wenyeji Ruvu Shooting watakapocheza na Mgambo JKT.

Hadi sasa Yanga ndio wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 4 mbele ya Mabingwa Watetezi Azam FC ambao wamecheza Mechi moja zaidi.

LIGI KUU VODACOM MATOKEO:
Jumamosi Aprili 18
Polisi Moro 2 Ndanda FC 0
Mbeya City 2 Simba 0
Azam FC 2 Kagera Sugar 1

LIGI KUU VODACOM RATIBA
Jumapili Aprili 19Ruvu Shooting v Mgambo JKT

About Author

Advertisement

 
Top