WALIOFARIKI KWA RADI MKOANI KIGOMA WAAGWA KWA MAZISHI MCHANA HUU.

Mazishi ya waliouwawa kwa radi kigoma
Miili ya Wanafunzi sita na Mwalimu ikiwa tayari kwa kuagwa katika viwanja vya shule ya Msingi Kibirizi mkoani Kigoma . WATU wanane wakiwemo wanafunzi sita na mwalimu wa shule ya msingi kibirizi mmoja pamoja na mtu wa kawaida mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapo walipoteza maisha hapo jana baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengine 15 kujeruhiwa na radi hiyo.
Mazishi ya waliouwawa kwa radi kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya akisoma salamu za rambi rambi za mkoa wakati wa kuaga miili ya Wanafunzi na Waalimu waliopigwa na radi jana.
Mazishi ya waliouwawa kwa radi kigoma
Katibu wa Bakwata mkoa wa Kigoma,Shekhe Moshi Guoguo akituma salamu za rambirambi kwa wafiwa.
Mazishi ya waliouwawa kwa radi kigoma
Wanajeshi wa JWTZ wakiingiza miili ya marehemu katika viwanja vya shule ya msingi Kibirizi kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Source:: Michuzi Media Group

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post