WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA NCHI YA ETHIOPIA 34 WAKAMATWA MKOANI LINDI, WAKIELEKEA AFRIKA KUSINI

Watu 34 wanaotajwa kuwa ni Raia wa Nchi ya Ethopia, wanashikilwa na jeshi la polisi mkoani hapa (LINDI) kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.
Afisa uhamiaji wa mkoa wa Lindi, Abdallah Towo ,amethibitisha kukamatwa watu hao. Ofisa huyo alisema watu hao walikamatwa mchana wakiwa wamejificha porini, katika mtaa wa Mmongo, Manispaa ya Lindi.

Towo amesema watu hao walikutwa katika eneo hilo wakiwa wamekaa na vifurushi vidogovido vikiwa na vyakula na maji. 
"walikuwa wanakwenda wapi lakini walikutwa wamekaa kwenye pori hilo, mtaa wa Mmongo," alisema Towo.

Alisema taratibu za kuwafikisha mahakamani wahamiaji haramu hao zinashugulikiwa, Ambapo wakati wowote watafikishwa mahakamani.

Naye kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, David Mafwimbo alithibitisha kukamatwa watu hao, nakuongeza kusema walikutwa kwenye pori hilo kwenye korongo.
"taarifa hizo ni zakweli, watu hao walikuwa wanataka kwenda Afrika ya kusini wamekutwa na vibegi na Vifuko vidogo vidogo vya chakula,"aliongeza kusema Mafwimbo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post