Unknown Unknown Author
Title: UMOJA AMCOS YAJIIMARISHA KIUCHUMI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz,Liwale Chama cha msingi cha ushirika UMOJA (UMOJA AMCOS) wilayani Liwale, mkoani Lindi. Kimefanikiwa kupata shilingi 127.06...
Liwale
Na Abdulaziz,Liwale
Chama cha msingi cha ushirika UMOJA (UMOJA AMCOS) wilayani Liwale, mkoani Lindi. Kimefanikiwa kupata shilingi 127.06 Milioni kutokana vyanzo vya mapato mbalimbali katika msimu wa 2014/20015.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa chama hicho, Hassan Mpako, kwenye taarifa yake aliyoisoma mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa 23 wa chama hicho, uliofanyika jana mjini Liwale.

Mpako alisema chama hicho kinaendelea kuimarika nakupata mafanikio makubwa ya kiuchumi kwani kimeweza kuwa na mali zisizohamishika na zinazo hamishika, zenye thamani ya shililingi bilioni 1. Ambapo pia kimeweza kulipa deni la fedha zilizotumika kujenga ghala la kuhifadhia mazao, ambalo ujenzi wake uligharimu shilingi 600.00 milioni.

"hakuna chama kinachotufikia kwa mafanikio haya tuliyoyapata kwa ukanda mzima wa kusini mwa Tanzania. Alisema katika msimu wa 2014/2015, chama hicho kilikusanya kilo 1357390 za korosho, ambazo zilikiizingizia shilingi 67.86 milioni.
Liwale Amcos
Aidha Kufuatia kushuka kwa kipato cha Mkulima wa zao la korosho wilayani Liwale licha ya zao hilo kuwa na soko Kubwa Duniani, Wito umetolewa kwa Wanachama wa Chama cha Msingi cha ushirika wilayani Liwale (UMOJA AMCOS) Kuanza mpango wa kukusanya zao hilo bila ya kukopa katika Taasisi za kibenki ili kuepuka Riba Kubwa ili kusaidia
kuongezeka kwa pato la wakulima baada ya Mnada wa Mauzo.

Wito huo Umetolewa Jana na Mkuu wa wilaya ya Liwale, Ephreim Mmbaga alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa 23 chama kikuu cha Umoja wilayani Humo na Kuhudhuriwa na wanachama 700 wa chama hicho Sambamba na Mkutano huo pia Wanachama wa umoja huo walipewa Taarifa la kukamilishwa kwa Deni la tshs Milioni 106 kati ya Milion 600
zilizotumika katika Ujenzi wa Ghala hilo.
Liwale Amcos
Kutokana na mafanikio hayo Wanachama wa chama hicho walichangia juhudi za Serikali katika ujenzi wa Maabara baada ya kukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Jumla ya Mifuko 50 ya Saruji ili kusaidia kukamilisha Ujenzi wa Vyumba 60 vya Maabara katika shule 20 za
Sekondari zilizo katika wilaya Hiyo.

About Author

Advertisement

 
Top