TANZANIA YATAJWA MIONGONI MWA MATAIFA 10 YANAYOKUWA HARAKA

LIU GUIJIN
Balozi LIU GUIJIN

TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa mataifa kumi yanayokuwa kwa haraka duniani kutokana na kuwa na Amani na utulivu, utawala bora pamoja na mwendelezo wa sera thabiti za maendeleo.

Hayo yamesemwa na balozi LIU GUIJIN aliyewahi kuwa balozi wa CHINA katika mataifa ya ZIMBABWE na AFRIKA KUSINI, wakati akifungua mjadala wa AMANI na MAENDELEO ambao umefanyika katika chuo kikuu cha BEIJING.

Kwa upande wake DR LAMIN SISSE aliyekuwa mshauri mkuu wa masuala ya kidiplomasia wa katibu mkuu wa zamani wa wa umoja wa mataifa KOFFI ANNAN, amesema imefika wakati kwa mataifa ya AFRIKA kuamua kusimama yenyewe bila kutegemea masaada wa mataifa mengine katika maendeleo.

Ameongeza kuwa matatizo ambayo mataifa mengi ya AFRIKA yanapitia ikiwemo vita za wenyewe kwa wenyewe iwe chachu ya kupata maendeleo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post